Ukumbi wa Uwekezaji

Maelezo ya Muwekezaji

Freelancer Limited

Freelancer ni soko kubwa zaidi la ufanyikazi huru na soko la watu wengi kwa idadi ya watumiaji na miradi. Freelancer ilianzishwa mnamo 2009 na imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Australia (ASX: FLN) na Masoko Bora ya OTCQX huko nchini Marekani (OTCQX: FLNCF).

Bei ya Hisa

Bei yetu ya sasa ya hisa inaweza kupatikana hapa:

Matangazo ya Kampuni

Kwa orodha kamili ya matangazo ya hivi karibuni ya kampuni tafadhali tembelea:

Kuwekeza Kutoka Nchi Marekani

Madalali wafuatao hufanya biashara ya hisa za OTC. Alama ya saa kwa Freelancer ni FLNCF.

Kuwekeza Ukiwa Australia

Alama ya ticker kwa Freelancer ni FLN.

Orodha kamili ya madalali wa hisa wa Australia na habari zingine juu ya kununua au kuuza hisa kwenye ASX zinaweza kupatikana hapa:

https://www2.asx.com.au/investors/start-investing/find-a-broker-adviser/full-service-and-online-brokers

Kuwekeza Kutoka Nchi Nyingine

Kwa watumiaji wote wa kimataifa, madalali wafuatao wanauza hisa za ASX. Alama ya tiki ya Freelancer ni FLN.

Kudhibiti Hisa Zako

Ingia kwenye tovuti ya Usajili wa sehemu ya Boardroom ili uone habari juu ya hisa zako za Freelancer. Boardroom inaweza kuufukiwa kwa kutuma barua pepe enquiries@boardroomlimited.com.au. Wanaweza kuwasiliana kwa simu kwa 1300 737 760 (ndani ya Australia) au + 61 2 9290 9600 kwa Ofisi ya Australia.

Maswali yaulizwayo ya Wawekezaji

Nawezaje kuwekeza?

Unaweza kununua hisa za Feelancer kupitia muuzaji hisa anayeungwa mkono kwenye Soko la Hisa la Australia (ASX). Jina la Freelancer ni ASX:FLN. Unapaswa kuitisha ushauri kutoka kwa mtaalam wa huduma za kifedha kabla ya kuwekeza.

Nitampataje muuzaji hisa?

Orodha kamili ya wauzaji hisa wa Australia na maelezo mengine kuhusu ununuzi na uuzaji wa hisa kwenye ASX unapatikana kwenye tovuti ya ASX. Hisa za Freelancer kwa kawaida zinaweza tu kununuliwa kupitia kwa muuzaji hisa aliyesajiliwa na ASX, kwa hivyo ikiwa wewe sio mkaazi wa Australia, itakubidi utafute mipangilio mingine. Interactive Brokers ni muuzaji hisa wa mtandaoni anayesajili wakaazi wa nchi mbali mbali ulimwenguni na anayeruhusiwa kuuza hisa kwenye ASX. Hata hivyo, unaweza pia kuwasiliana na muuzaji hisa wako kuona ikiwa ana uhusiano na muuzaji hisa aliyesajiliwa kwenye ASX.

Je watumiaji wa Freelancer.com ambao pia ni wawekezaji wa Freelancer wanapokea manufaa zaidi?

Ndiyo. Freelancer imetunga mpango maalum wa Foundation ya Wawekezaji unaotuza watumiaji walioshikilia kiwango kidogo mno cha hisa. Kwa maelezo zaidi, tembelea Ukurasa wetu wa Mpango wa Foundation ya Wawekezaji.

Nitapata wapi matangazo ya kampuni?

Matangazo ya sasa na ya awali ya kampuni yanapatikana kwenye tovuti ya ASX na pia kwenye sehemu ya Matangazo ya Kampuni ya tovuti ya Freelancer.

Ni lini Freelancer itatoa matangazo ya kampuni yatakayoathiri hisa zangu?

Freelancer itajaribu kuwashauri wawekezaji wake kuhusu tarehe zinazotarajiwa za kutumwa kwa matangazo muhimu kwenye sehemu ya Maelezo ya Mwekezaji ya tovuti yake.

Nitapata wapi maelezo ya kihistoria ya bei za hisa?

Bei zetu za sasa na za awali zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya ASX. Ili kutafsiri maelezo ya bei ya hisa, wawekezaji wanashauriwa kutafuta ushauri wa wataalam.

Nitatazama vipi uwekezaji wangu kwenye FLN?

Unaweza kutazama maelezo yako ya sasa kuhusu uwekezaji wako kwenye Freelancer kupitia tovuti ya saraka ya hisa ya Boardroom.

Nawekaje upya maelezo yangu ya uwekezaji?

Ingia kwenye tovuti ya Boardroom ya saraka za hisa ili uweze kutazama maelezo ya hisa zako za Freelancer na kuweka upya maelezo yako.

Nitapataje maelezo ya uwasilianaji ya saraka za hisa za Freelancer?

Maswali yote kuhusu maelezo ya uwekezaji yanapaswa kuelekezwa kwa Boardroom. Boardroom inaweza kufikiwa kwa kutuma pepe kwa enquiries@boardroomlimited.com.au. Unaweza kupiga simu kwa 1300 737 760 (ndani ya Australia) ama +61 2 9290 9600 kwa ofisi ya Australia.

Ripoti na Maonyesho

Mpango wa Freelancer wa Foundation ya Wawekezaji

Mpango wa Freelancer Foundation Shareholder unawapatia wawekezaji wa Freelancer Limited (ASX:FLN) manufaa fukani ikiwemo bei zilizopunguzwa kwa baadhi ya huduma za Freelancer.

Mwanahisa wa Freelancer

Manufaa kwa Mtazamo

Kurudishiwa Ada kwenye Freelancer.com

Punguzo la asilimia 5% la mradi na marupurupu ya shindano litatumwa kwenye akaunti yako ya Freelancer.com, na itapigwa hesabu ya kila mwezi, kwa kila mwezi mzima ambao utasalia kwenye mpango.

Huduma ya Kipekee kwa Wateja

Utapokea huduma ya kipekee kwa wateja kutoka kwa timu yetu 24x7x365

Baji ya Mwekezaji wa Freelancer Foundation

Baji ya kipekee itaonekana kwenye profaili zako za Freelancer.com na WarriorForum, hivyo basi kuashiria kuwa wewe ni mwekezaji wa kampuni.

Fikia Manufaa Yako

Manufaa haya yanapatikana kwa watu binafsi walio na angalau hisa 5,000 za kawaida zinazolipwa kikamilifu za Freelancer Limited. Bofya tu kitufe kilicho hapa chini na ujaze fomu ya maombi ili kuanza kufikia manufaa yako.

Mahali pa Kununua Hisa

Alama ya tiki ya Freelancer ni ASX:FLN kwa mtu yeyote anayenunua hisa kutoka Australia. Kwa watumiaji wote wa kimataifa nje ya Australia, unaweza kufanya biashara ya hisa za ASX:FLN kwenye Tiger Brokers.

Sheria na Masharti

Ndiposa uhitimu kuwa kwenye Mpango wa Freelancer Foundation Shareholder, ni sharti uwe na yafuatayo:

 • Ni sharti muwekezaji awe mwanachama aliyesajiliwa kwenye tovuti za aidha Freelancer.com ama Warrior Forum (Mtumiaji wa Freelancer). Akaunti zilizositishwa hazitaruhusiwa. Watumiaji wa Freelancer wanaokiuka Sheria za Utumiaji za aidha ya tovuti hizo mbili (kama ilivyoelezewa kwenye Makubaliano ya Utumiaji) wataweza kusitishiwa uanachama wao kwenye Mpango ama hata kufutiliwa mbali, kama itakavyoamuliwa na Freelancer Limited.
 • Mwenyehisa lazima awe mtu/watu wa asili na:
  • anamiliki hisa 5,000 za kawaida zilizolipwa kikamilifu za Freelancer Limited; au
  • imeteuliwa na kampuni, amana au shirika lililojumuishwa ambalo linamiliki hisa 5,000 za Freelancer Limited za kawaida zilizolipiwa Kampuni, shirika la uaminifu au shirika lililojumuishwa linaweza kuteua mtu mmoja wa asili kupokea manufaa kamili ya kifurushi kinachotumia fomu ya Ushauri ya Kuteuliwa Kwa Mteule (Nominee Appointment Advice form - pdf), na nakala yake iliyochanganuliwa lazima iambatanishwe na fomu ya maombi mtandaoni. Fomu tofauti ya uteuzi lazima ijazwe ambapo zaidi ya shirika moja limesajiliwa katika umiliki wa pamoja.
   • Mwanahisa lazima awe na hisa 5,000 za kawaida zinazolipwa kikamilifu za Freelancer Limited kwa mwezi mzima wa kalenda ili kustahiki manufaa ya wanahisa katika mwezi huo wa kalenda. Mapunguzo ya ada hayatalipwa kwa mwezi wowote na mapunguzo ya ada hayatapatikana ambapo hisa za mwenyehisa zinaanguka chini ya hisa 5,000 za kawaida zinazolipwa kikamilifu za Freelancer Limited.
   • Punguzo hulipwa kwenye mradi ama mashindano (sio viboresho), na kwa ada tu zilizolipwa. Ada ambazo hazijalipwa hazitaweza kupokea punguzo.
   • Freelancer Limited itaweza kubadilisha manufaa, sheria na masharti ya Mpango wa Freelancer Foundation Shareholder kwa wakati wowote, pamoja na kuweka upya ukurasa huu.