Ada na Malipo ya Freelancer

Kwa Waajiri

Miradi

Freelancer haina malipo kujisajili, kuchapisha mradi, kupokea zabuni kutoka kwa wafanyikazi huru, kupitia kwingineko ya mfanyikazi huru na kujadili mahitaji ya mradi. Ikiwa unachagua kutuza mradi, na mfanyikazi huru akubali, tunakulipisha ada ndogo ya mradi kulingana na thamani ya zabuni iliyochaguliwa, kama ada ya utangulizi.

Gharama na jinsi ada hii inatozwa inalingana na aina ya mradi.

Kwa miradi isiyobadilika bei, ada ya 3% au $3.00 USD (iliyo juu kati yazo) inatozwa ambapo mradi ulioutuza umekubaliwa na mfanyikazi huru mwenye uliyemtuza. Ikiwa wewe baadaye utamlipa mfanyikazi huru zaidi ya kiasi asili cha zabuni, tutatoza ada ya mradi kwa malipo yoyote ya ziada.

Kwa miradi ya kila saa, ada ya 3% inatozwa kwa malipo yote utakayofanya kwa mfanyikazi huru.

Unaweza kubatilisha mradi kutoka kwenye dashibodi wakati wowote hadi siku saba (7) baada ya mradi kukubalika ili urudishiwe ada yako yote.

Viboresho vya shindano visivyo vya lazima vinaweza kununuliwa.

Mashindano

Wakati wa kuchapisha shindano, waajiri wanapaswa kutoa fedha sawa na jumla ya zawadi ya shindano. Tuko na Dhamana ya Kurudishiwa Pesa kwa fedha hizi za tuzo.

Uhakikisho wa kurudishiwa fedha unakuwezesha kurudishiwa fedha hadi kwa siku 30 baada ya shindano kufungwa ikiwa hautafurahishwa na wasilisho zilizotumwa. Utaweza kurudishiwa ikiwa ku wasiliana na huduma.

Kumbuka kuwa kurudishwa kwa fedha hakuko kwenye 'Mashindano yaliyohakikishiwa', na kurudishwa huku hakujumuishi viboresho vyovyote ulivyochagua vya shindano. Ikiwa tayari umeshachagua wasilisho kama la ushindi na kukamilisha ukabidhi wa shindano, ambayo itawachilia fedha, hautahitimu kurudishiwa fedha zozote.

Hakuna ada ya kutuma na kutuza shindano kwa waajiri.

Kila wasilisho la ziada litahitaji malipo ya zawadi ya wasilisho hilo.

Viboresho vya shindano vinaweza kununuliwa.

Huduma

Wakati wa kuomba huduma, waajiri ni sharti watoe fedha zilizo sawa na jumla ya bei ya huduma ile. Malipo hayo yamelindwa na Mfumo wa Freelancer wa Malipo ya Hatua. Wachilia tu malipo unaporidhika kwa 100% na kazi iliyowasilishwa.

Kwa Wafanyakazi huru

Freelancer haina malipo kujisajili, kutunga profaili, kuchagua ujuzi wa miradi inayokuvutia, kupakia kwingineko, kupokea vijulisho vya mradi, kujadiliana maelezo ya mradi na muajiri, kuweka zabuni kwenye miradi (wanachama wa bure kwa awali hupokea zabuni 6 kwa mwezi) na kuingia kwenye mashindano.

viboresho vya zabuni vya hiari vinaweza kununuliwa kudhamini zabuni.

Miradi

Kwa miradi isiyobadilika bei, ikiwa utatuzwa mradi, na uukubali, tunakutoza ada ndogo ya mradi mkabala na dhamani ya zabuni iliyochaguliwa, kama ada ya utambulisho. Ikiwa baadaye utalipwa zaidi ya kiasi asili cha zabuni, tutatoza ada ya mradi kwa malipo yoyote ya kadri.

Kwa miradi ya saa, ada inatozwa kwa kila malipo kama inavyofanywa kwa mfanyakazi huru.

Ada kwa mradi isiobadilisha bei ni 10% au $5.00 USD, inayozidi nyingine, na 10% kwa miradi ya saa.

Mashindano

Kutuma wasilisho kwenye shindano ni bure. Ada za shindano zinatumiwa wakati unatuzwa zawadi ya shindano. Ada hii inatozwa wakati zawadi inawachiliwa, ambayo ni baada ya wewe kutuzwa shindano na ukabidhi wa vifaa vya wasilisho umekamilika na aliyetuma shindano awe ameridhika.

Ada ya freelancer ya shindano ni 10% ama $5.00 USD, kati ya hizo iliyo juu.

Huduma

Ikiwa baadaye utaajiriwa kutoa huduma hii, ada ya asilimia 20% ya jumla ya bei ya huduma itatozwa. Hii itatozwa wakati ombi la huduma linawasilishwa huduma inaitishwa kutoka kwa malipo utakayopokea.

Mfumo wa mwanahuru anayeaminika

Ikiwa uko kwenye Mpango wa Preferred Freelancer, utatozwa ada ya mradi ya asilimia 15% wakati unapotuzwa na kukubali mradi wa Mwajiri. Hii haitatanguliwa kutozwa namna ilivyo kwenye miradi za kawaida, bali hadi utakapopokea malipo.

Marejesho kama Mkopo wa Bonasi

Wakati mwingine, kurudishiwa ada kutafanyika kama marupurupu ya credit. Marupurupu haya yanaweza tu kutumiwa kwenye tovuti, na hayawezi kutolewa ama kuhamishwa. Muda wa marupurupu utaishi katika siku 90 tangu yalipopeanwa.

Promosheni ya Ada 0%

Ada za ujira za Freelancer zinazotozwa kwa wafanyakazi huru wanaowaelekeza waajiri wasio na akaunti kwenye Freelancer.com na wanaojiunga na kutunga akaunti mpya, zitapunguzwa kutoka 10% hadi 0%, kwa miradi zote za usoni zinazofanywa na mfanyakazi huru aliyeelekeza kwa muajiri aliyeelekezwa.

Hii italingana na mambo yafuatayo:

 • Waajiri wapya ni sharti waelekezwe kwa kutumia anwani maalum za uelekezi kwenye https://www.freelancer.com/no-commission.
 • Kwa kuondoa tashwishi, ada ya ujira iliyopunguzwa ya miradi ya freelancer ya 0% inatumiwa kwa kazi mpya inayofanywa na mfanyakazi huru aliyetuma ombi kikamilifu kumhusu muajiri fulani ambaye ada hizi zinahusiana. Miradi hiyo mipya ni sharti ianze baada ya muajiri kutunga akaunti mpya kwenye Freelancer.com na aanze kutumia akaunti hiyo.
 • Ada za mradi za ujira kwa mfanyakazi huru zinapunguzwa kuanzia 10% hadi 0% kwenye toleo hili. Ada nyingine na malipo hazitabadilika zikijumuisha ingawa sio tu, ujira kwa muajiri na ada za matumizi.
 • Promosheni hii haiko kwa mashindano.
 • Freelancer ina idihini ya kukaguwa waajiri kama waajiri wapya kwa minajili ya toleo hili, ili kuhakikisha utumizi mzuri wa toleo hili. Waajiri ni sharti wawe washawahi fanya kazi. na kumlipa mfanyakazi huru kabla ya kuanza kwa toleo hili, kwa mfano kwenye tovuti nyingine. Wafanyakazi huru wanaweza kuombwa kutoa ushahidi wa kazi ya awali na malipo kabla ya kuhitimu kupunguziwa ujira. Ndiposa wahitimu, waajiri ni sharti wasiwe waliwahi kuwa na akaunti kwenye Freelancer.com ambako malipo yaliwahi kufanywa katika miezi 6 kabla ya kutengeneza akaunti hii mpya.
 • Mambo mengine yote ya Makubaliano ya Utumiaji yanaendelea kutumika - tazama https://www.freelancer.com/about/terms.
 • Mambo mengine yote ya Ada na Malipo ya Sheria Zaidi yanaendelea kutumika - tazama https://www.freelancer.com/feesandcharges.
 • Freelancer inaweza kuhitaji kuwa wahusika wote wajaze na kukamilisha profaili zao na/ ama wafaulu katika ukaguzi wa utambulisho kabla malipo yawachiliwe.
 • Freelancer inaweza kuhitaji kuwa maelezo ya mradi wowote ambao kupunguzwa kwa ada kunatumika yawe yamekamilika kabisa.
 • Toleo hili litaondolewa kwa mtumiaji fulani ikiwa kurudishwa kwingi, ulaghai ama kudai zilizolipwa kunaonekana, ikiwa Freelancer inaamini kuwa kuna uwezekano wa hasara wa fedha kurudishwa ama kudaiwa, kutokana na migogoro kati ya muajiri na mfanyakazi huru, ama kwa sababu ile yoyote.
 • Freelancer ina idihini ya kuzuia utumizi wa toleo hili kwa kuamua kwake mwenyewe, kulingana na utumiaji ufaao wa toleo hili, na kuzuia ulaghai wowote unaoshukiwa.
 • Freelancer ina idihini ya kuhitaji kuasilishwa kwa maelezo zaidi kutoka kwa mhusika yeyote ambaye atatuma ombi la kutumia tooleo hili, ili kuchunguza ulaghai na kudhibiti hasara na sababu husika.
 • Freelancer ina idhini ya kubatilisha ama kubadilisha toleo hili kwa wakati wowote.
 • Freelancer ina idihini ya kubatilisha toleo katika eneo lolte ikiwa litakisiwa ama itakuwa kinyume cha sheria kumpatia mtu yeyote anayeishi katika eneo hilo.

Mipango ya Uanachama

Chagua kati ya mipangilio ya uanachama ili kuamua ada utakayolipa kwenye huduma hii. Unaweza kufanya kazi kwenye tovuti kama muajiri ama mfanyakazi huru kama mwanachama wa bure, ama upokee manufaa zaidi kama mwanachama wa kulipwa kwa kuboresha hadi kwa mpango wa kulipwa

Uanachama utarudiwa kila mwezi ama kwa mwaka kila tarehe ulipojisajili ifikapo, ikiwa haitabatilishwa. Ikiwa fedha hazitatosha, tutajaribu kuweka uanachama wako hadi kwa siku 30 hadi fedha zitakapopatikana.

Unaweza kubatilisha uanachama wako wakati wowote kupitia ukurasa wa mipangilio ya mtumiaji, ambayo itasitisha utozaji mwishoni mwa muda wako wa usajili bila gharama zaidi.

Tazama mipango yetu ya uanachama

Ada Nyingine

Miradi

Ada zifuatazo hutozwa kwa hiari kwa huduma za ziada. Isipokua imeainishwa vinginevyo kulingana na manufaa ya mpango wa uanachama wa kulipiwa:

Kutuma Mradi BURE
Il'ohusishwa $9.00 USD
Dharura $9.00 USD
Ya Kibinafsi $19.00 USD
Wakati Wote $199.00 USD
Muajiri $9.50 USD
Makubaliano ya Kutotoa Taarifa (NDA) $19.00 USD
Makubaliano ya IP $19.00 USD
Imefichwa $9.00 USD
Kipaumbele $5.00 USD
Ongeza muda $9.00 USD

Mashindano

Ada zifuatazo hazitozwi kwa lazima kwa huduma zaidi. Labda iwe imebainishwa wazi kulingana na manufaa ya mpango wa uanachama wa kulipiwa:

Kutuma Shindano BURE
Kutuza shindano BURE
Kutuzwa kwa wafanyakazi huru wengine BURE
Imehakikishiwa BURE
Il'ohusishwa $30.00 USD
Shindano Kuu $30.00 USD
Dharura $35.00 USD
Onyesha $15.00 USD
Imefichwa $30.00 USD
Ya Kibinafsi $25.00 USD
Makubaliano ya Kutotoa Taarifa (NDA) $20.00 USD
Ongeza muda Gharama:
Siku 3 = 15% ya zawadi ya shindano
Siku 5 = 20% ya zawadi ya shindano
Siku 7 = 30% ya zawadi ya shindano
Siku 14 = 40% ya zawadi ya shindano
Siku 21 = 50% ya zawadi ya shindano
Nusu ya gharama itatumiwa kuongeza bei ya shindano (na kugeuzwa iwe nambari kamili).

Ada ya Zabuni

Kuzabunia miradi BURE
Zabuni Iliyodhaminiwa Asilimia 0.75% ya kiwango cha zabuni (kiasi cha chini $5.00 USD, kiasi cha juu $20.00 USD)
Onyesha Zabuni $1.00 USD

Ada za Kuwasilisha Shindano

Tuma Wasilisho BURE
Wasilisho Lililofichwa $0.50 USD
Onyesha Wasilisho $0.50 USD

Ada za Saraka

Udhamini wa saraka Kama ilivyochaguliwa wakati wa kudhamini (ya chini $50.00 USD)

Mitihani

Kufanya mtihani Inalingana na mtihani. Kama ilivyofafanuliwa kabla ya kununuliwa. Kawaida inaweza kuwa bure,$5.00 USD, $10.00 USD, ama $15.00 USD.

Ada ya Matumizi

Ada za matumizi zilizotozwa kwa kutumia Kadi ya Mkopo, PayPal ama Skrill.* $0.30 USD + 2.3%
Kuweka kwa Benki BURE
Uhamisho wa Kimataifa $15.00 USD
*Watumiaji wa Australia watatozwa $0.30AUD + 0.99% ya utumiaji wa kadi ya malipo.

Ada ya Utatuzi

Ada ya utatuzi kwa mgogoro wa hatua ni $5.00 USD ama 5%, kati ya hizo iliyo juu.

Mfumo wetu wa utatuzi umebuniwa kuwawezesha wahusika wote kutatua shida kuhusu malipo ya hatua kati yao bila utatuzi wa nje.

Siku 4 baada ya mgogoro kuanzishwa (ama siku 7 ikiwa mgogoro utawasilishwa na mfanyakazi huru) mmoja kati ya wahusika anaweza kuchagua kuelekeza mgogoro utatuliwe na waamuzi wa kulipwa. Mhusika mwingine asi atakuwa na siku 4 zaidi kukubali kulipa ada hii na kwa wahusika wote kuwasiisha ushahidi wa mwisho. Ikiwa mhusika huyo mwingine atashindwa kulipa kwa wakati ufao, basi atapoteza mgogoro.

Kisha ada ya utatuzi itarudishiwa mshindi wa mgogoro.

Ada za Kutoa

Ada zitatozwa kulingana na mbinu ya utoaji. Ada za ziada zinaweza kutozwa na mhusika anayepeana mbinu hiyo ya kutoa.

Kutoa kwa Express BURE
PayPal BURE
Skrill (Moneybookers) BURE
Kadi ya Malipo ya Payoneer BURE
Uhamisho wa Kimataifa $25.00 USD

Tunasisitiza kiasi cha kutoa cha chini kiwe, baada ya ada, USD $30.

Ada ya Ulinzi

Akaunti za Utumiaji ambazo hazijatumiwa mtandaoni kwa miezi sita zitatozwa ada ya ulinzi ya hadi $10.00 USD kwa mwezi hadi wakati akaunti itafungwa ama ifunguliwe tena, na itakuwa ada itakayogharamia uwekaji, data, huduma na udhibiti unaofanyika kwenye profaili ya mtumiaji, uwekaji wa portfolio, kuwekwa katika saraka, utoaji wa huduma za Niajiri, uwekaji faili na uwekaji wa ujumbe. Ada hizi zitaweza kurudishwa ikiwa mtumiaji ataomba, ilimradi akaunti ifunguliwe tena.

Ushuru

Ushuru hutumiwa kulingana na viwango vya ndani na sheria zilizoainishwa na nchi ya mtumiaji / nchi iliyosajiliwa.

Australia - Ushuru wa Bidhaa na Huduma (GST) 10%
Uchile - Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) 19%
Jumuiya ya Ulaya - Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) VAT rates
India- Ushuru Unaokusanywa kwenye Chanzo (TCS) 1%
Uhindi - Ushuru Umepunguzwa kwa Chanzo (TDS) 1% / 5%
Mexico - Zuio la Ushuru wa Mapato 1% / 20%
Mexico - Ushuru wa Kuongeza Thamani (VAT) 16%
Urusi - Kodi ya Nyongeza Thamani (VAT) 16.67%
Uswizi - Kodi ya nyongeza Thamani (VAT) 7.7%

Marejesho ya Ushuru wa Usawanishaji wa India

Ili kuepusha shaka, mkataba huo unawaondolea wafanyikazi huru jukumu la kuzuia Ushuru wa Usawazishaji.

Mteja Mfanyakazi Huru Nani Hulipa Ushuru Maelezo ya Ushuru
Mkazi wa India Mkazi wa India Mfanyakazi Huru 2% inatozwa kwa Mfanyikazi huru kwa jumla ya mapato
Mkazi wa India Nyingine Mteja 2% inatozwa kwa Mteja kwa jumla ya malipo ya hatua.
Nyingine Mkazi wa India Mfanyakazi Huru 2% inatozwa kwa Mfanyikazi huru kwa jumla ya mapato
Nyingine Nyingine Haitumiki Haitumiki

Client

Mkazi wa India

Freelancer

Mkazi wa India

Who Pays Levy

Mfanyakazi Huru

Maelezo ya Ushuru

2% inatozwa kwa Mfanyikazi huru kwa jumla ya mapato

Client

Mkazi wa India

Freelancer

Nyingine

Who Pays Levy

Mteja

Maelezo ya Ushuru

2% inatozwa kwa Mteja kwa jumla ya malipo ya hatua.

Client

Nyingine

Freelancer

Mkazi wa India

Who Pays Levy

Mfanyakazi Huru

Maelezo ya Ushuru

2% inatozwa kwa Mfanyikazi huru kwa jumla ya mapato

Client

Nyingine

Freelancer

Nyingine

Who Pays Levy

Haitumiki

Levy Details

Haitumiki

* Freelancer na washirika wake haitoi ushauri wa ushuru, sheria au uhasibu. Nyenzo hii imeandaliwa kwa sababu ya habari tu, na haikusudiwi kutoa, na haipaswi kutegemewa kwa ushauri wa ushuru, sheria au uhasibu. Unapaswa mwenyewe kushauriana na washauri wako wa ushuru, sheria na uhasibu.

Makubaliano ya Utumiaji

Ada na malipo yaliyoandikwa kwa mukhtasari kwenye ukurasa huu yanaongozwa na Makubaliano ya Utumiaji na sera husika za tovuti za Freelancer . Makubaliano ya Utumiaji yanajumuisha sheria nyingine muhimu na yanapaswa kusomwa yote. Haswa sehemu ya 23 ya Makubaliano ya Utumiaji inaelezea adhabu ya kusitishwa kwa kukiuka Makubaliano ya Utumiaji. Adhabu hiyo inajumuisha faini kuhusu madhara ambayo Freelancer itakumbana nayo kutokana na vitendo vitakavyokiuka Makubaliano ya Utumiaji.